Tunajua kuwa maradhi ya ngozi huwaathiri watu kwa muda mrefu, lakini hojaji hii inanuia kupima kiwango ambacho maradhi ya ngozi yamekuathiri kimaisha KWA MWEZI ULIOPITA. Tafadhali jibu kila swali kuhusiana na maradhi yako ya ngozi. Tafadhali chagua kisanduku kimoja pekee kwa kila swali. Tumetoa mifano ili kukupa wazo kuhusu mambo ya kuzingatia. Mifano hii ni kielelezo tu wala haipaswi kuwa kizuizi kwa majibu yako. Maradhi ya ngozi yanaweza kuathiri ngozi, nywele, kucha na/au utando telezi. Neno ‘ngozi’ hapa linajumuisha chochote kati ya vipengele hivi vinavyohusiana na maradhi yako.
Tafadhali hakikisha kuwa umejibu kila swali.
Asante.